Wednesday, May 28, 2014

FASHION MAKALA || KiKi, Model mpaka ‘KiKi FASHION’.

Kiki Zimba, ni mwanadada ambae ni mama mwenye watoto na familia yake nzuri sana ambao wanaishi jijini Dar Es Salaam, alianza kazi zake za fashion miaka mingi sana na nadhani hiyo ndio imeweza kumsaidia kuweza kufanya kazi zake kuwa nzuri zenye ubunifu na za ufanisi zaidi sababu ukizungumzia ustadi wa kitu chochote sio kila mtu anaweza kufanya kila kitu. Kiki alikuwa mmoja kati ya wanadada waliokuwa kwenye “Modeling Industry” miaka ya 90 na kufanya kazi kwenye agency moja na wanamitindo wakubwa toka hapa nchini kama ‘Miriam Odemba’ ambe alifika na mpaka leo yupo ngazi za juu kimataifa kwenye kazi hizo za uanamitindo.

 Kiki akiwa kama Model kwenye agency ya kwanza kabisa Tanzania iliyokuwa inajulikana kama ‘Faces International’ iliyokuwa chini ya mwanamama Late. AMINA MONGI ambae alifariki katika ajali ya gari akitokea mjini Moshi mwaka 2000, tunaweza tukasema ukizungumzia Modeling na Fashion industry ya Tanzania lazima jina lake litajwe.

Kiki alianza na biashara ya Boutique baada ya dreams za kati ya vijana wengi wa kampuni hiyo kuwa “models” kuishia baada ya usimamizi wa ‘Faces International’ kuanza kutokueleweka baada ya Kifo cha Marehemu Amina Mongi. Alifungua ‘KiKi’s Boutique’ na kuanza kufanya safari za China na America kununua nguo za aina mbali mbali na kuja kuuza kwenye duka lake. Hivi sasa KiKi anatengeneza nguo zake mwenyewe ambazo zimekuwa gumzo kwa wanadada wanaoheshimika hapa nchini na wakina mama ambao wanaelewa Fashion ni nini. 

For more story go to:www.gongamx.com