Nyalandu’s Love, Integrity and Power.
“Mkipendana, mkiaminiana maisha hayatoweza kuwatatiza. Na hata kama nikisikia neno kwa mfano leo hii au hata kesho kwangu mimi kwanza natambua kwamba yeye ni kiongozi wa kitaifa, kiongozi wa nchi yetu na ni kiongozi wa familia yangu kwahiyo jambo likisemwa, mara nyingi sana narudi nyuma na kumwangalia yeye kwa mimi ninavyomfahamu , mimi kama mke wake na naamini kwamba mimi namfahamu vilivyo pengine labda katika wanawake ukiacha mama yake mzazi, mimi hapa ndio ninamfahamu sana kuliko wanawake wote,” alisema Faraja kwenye mahojiano hayo.